MAPENZI
1. MWANAMKE MBEA.
Ni mwanamke anayependa kuongea mambo ya watu na hasa mambo mabaya. Mwanamke wa aina hii huwa anamfikirisha sana mpaka mume wake kutamani asimsikilize.
2. MWANAMKE GOGO KITANDANI.
Analala kama amekufa akisubiri mwanaume ndiye awe wa kumchochea au kumpa hamasa. Suala ili huwa linampa kila mwanaume maswali mengi kichwani.
3. MLALAMIKAJI.
Hakuna jambo zuri mbele yake. Ni mwepesi wa kumnyoshea kidole mume kwamba ndiye mkosaji. Hii huwa inamfanya mwanaume kujiona hana maana na hana msaada kwako.
4. ASIYEJIKUBALI.
Muda wote anaangalia chini . Kila mara anaona kakosa yeye na ni wa kuomba msamaha. Hata mwanaume akimwambia wewe ni mzuri anakuwa haamini. Mwanamke wa aina hii hata kama ni mzuri atakuwa mbaya tu .
5. ANAYEJITEGEMEA.
Mwanamke mwenye uwezo wa kujifanyia mambo yake ,hahitaji msaada wa mwanaume . Hata, mwanaume akitokea kutaka kuonyesha mapenzi hapa lazima atafukuzwa.
6. MWANAMKE MVIVU.
Anapenda kufanyiwa kila kitu . Ni mwanamke ambaye hana maono na mipango ya maisha ya mbeleni. Mwanamke golikipa,mpaka mwanaume alete tu. Mwanamke mwenye tabia hii ni kero kwa mwanaume.
7. MSHIKA DINI.
Huyu kila jambo zuri huwa anasema ni la shetani. Hana furaha na ndoa kwasababu yeye hata tendo la ndoa analihesabu kama uzinzi.
8. MWENYE HASIRA ZA HARAKA.
Ni mkali kwa kuongea hata kama anaongea na watoto au mume wake. Hana amani na mtu. Mazungumzo kidogo tu kwake yeye ni mjadala na lundo la maneno.
9. MWENYE MZAHA AU UTANI.
Huyu anamchekea kila mtu na anataniwa mpaka kushikwa sehemu nyeti na anaona kawaida hata kama kaolewa.