MICHEZO
Misri ipo katika hatua nzuri za kumnasa kocha Herve Renard kwaajili ya kuinoa timu yao ya Taifa ambayo imekuwa na msimu mbaya kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika nchini Côte d’ivoire .
Uongozi wa chama cha soka Misri (EFA) unaripotiwa kuwa kwenye mazungumzo ya mwisho ya kumpa kandarasi Renard ambaye amekuwa kocha wa timu ya taifa ya wanawake kuwa kocha wa timu ya wanaume.
Uamuzi wa kumpa kandarasi Herve Renard umekuja tu baada ya kusitisha mkataba na kocha wao Rui Vitoria kufuatia timu yao kutolewa kwa hatua ya 16 bora ya michuano ya Afrika dhidi ya DRC .
Herve amekuwa na mwendelezo wa mafanikio kwa kuzisaidia timu mbili tofauti za Mataifa tofauti kutwaa kombe la michuano hiyo .mara ya kwanza 2012 akitwaa na Zambia na mwaka 2015 akatwaa na Tembo wakubwa ,Côte d’ivoire.
Kwenye michuano ya kombe la Dunia 2022, Herve Renard aliushtua Ulimwengu wa soka baada ya kuiongoza Saudia Arabia kuichapa Argentina 2-1 kwenye michuano iliofanyika nchini Qatar.