MICHEZO
Kama kuna kitu wasanii wa Nigeria walikuwa na uhakika nacho katika tuzo za 66 za Grammy 2024, ni kuondoka na ushindi mnono kutokana na kuchaguliwa kuwania vipengele vingi ,pamoja na kupewa kutumbuiza lakini wameangukia pua.
Tuzo hizo zilizoanzishwa mnamo mwaka 1959 mwezi Mei 4 zikifahamika kama Gramophone, zilitolewa mapema jumapili ya Februari 4,2024 kwenye bonge la ukumbi ujulikanao kama Crypto.com kwenye jiji la Los Angeles nchini Marekani huku wasanii wakubwa wakiwepo.
Burna Boy aliwania vipengele vinne,Davido vipengele vitatu,Ayra Starr na Asake wakiingia kwenye kipengele kimoja.
Burna Boy,Davido na wenzake watarejea kwao patupu huku jambo ili likiwapa wakati mgumu.
Nyota wa mziki wa Amapiano kutoka Afrika Kusini, Tyla,22 ndiye msanii pekee wa Afrika aliyeibuka kidedea akiwa mshindi kwenye kipengele cha “Best African Music performance ” huku akiwabwaga Asake, Davido, Ayra Starr na Burna Boy.
Ushindi wa Tyla umekuja baada ya siku za hivi karibuni, yeye kufunguka kuwa angeshinda ikiwa atachaguliwa kuwania tuzo hizo.