MICHEZO
Timu ya Taifa ya DRC inakwenda kutumia mchezo wa nusu fainali ya Mataifa ya Afrika AFRICON kutuma ujumbe wa pole kwa waathirika wa mapigano ya muda mrefu Kaskazini mwa nchi yao.
Wamesema hawatavaa jezi kwaajili ya kupata ushindi bali kutuma salamu za pole kwa waathirika wa mapigano na pia kuiomba Serikali na waasi kufika kwenye maridhiano.
Nahodha wa kikosi hicho cha Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Chancel Mbemba amechapisha ujumbe unaosema “Naomba mara kwa mara nchi yangu irudi kwenye utulivu ili watu waishi kwa amani”.
Eneo la Kaskazini mwa CONGO limekuwa uwanja wa vita kati ya Wanajeshi wa Serikali na Waasi wa M23 ambapo maelfu ya watu wamekufa na wengine kuikimbia nchi yao.
DRC itakipiga na mwenyeji timu ya Taifa ya Côte d’ivoire kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Mataifa ya Afrika mnamo Februari 7,2024 huku ikipambana kulitwaa kombe hilo kwa mara ya pili baada ya miaka 50 kupita.