MAPENZI
1. USIONGEE KAMA KWAMBA MTOTO HATAKIWI.
Usimfanye mkeo na mtoto wajione wametengwa,hata kama ujauzito uliingia bila mipango.
2. FANYA MAOMBI KWAAJILI YA MWANAO.
Usisubiri mpaka mtoto azaliwe,hata atakapokuwa tumboni muombee mwanao .
3. EPUKA KUCHEPUKA.
Pale mkeo akiwa mjamzito epuka kutembea nje ya ndoa yako kwani kufanya hivyo kutampa makasiriko mkeo na baadaye anaweza akazaliwa mtoto mwenye hasira.
4. JIFUNZE ZAIDI MASUALA YA MALEZI.
Hata akiwa sio mtoto wako wa kwanza ni vizuri kujifunza kuona ni vipi mtoto anatakiwa kufanyiwa na mzazi au wazazi wake.
5. USIMHUZUNISHE MKEO.
Usimfanye mkeo awe na huzuni kwani kufanya hivyo ni kumtia huzuni mwanao. Madhara ya kumhuzunisha mkeo ni pamoja na kuja kumsababishia mkeo matatizo kwenye kujifungua na hata suala la huzuni linaweza kusababisha mtoto azaliwe njiti.
6. MSAIDIE MKEO.
Mkeo anaweza kuwa na mambo mengi na pia wakati mimba inakuwa basi anakuwa anachoka,kwahiyo ni wakati sahihi kama mume kumsaidia katika shughuli mbalimbali.
7. USIMHUKUMU MKEO.
Wakati mwingine Mwanamke anapokuwa mjamzito huwa kuna baadhi ya tabia zisizo za kawaida ambazo huwa zinafanywa na Mwanamke. Kwahiyo Mwanamke akibadilika kitabia ni Wakati mzuri kama mwanaume kumuelewa kuwa yuko kwenye mabadiliko.
8. ZUNGUMZA NA MKEO.
Muulize kama yuko vizuri? Muulize kama anaogopa? Muulize kama anatokwa na majimaji kwenye uke? Muulize kama ana shinikizo la damu? Hali ya kichanga tumboni? Amejiandaaje kuwa mama? Haya ni baadhi ya maswali.
9. USIOMBE TENDO LA NDOA.
Ukibahatika mkeo akawa yuko huru Kufanya hivyo ni vizuri lakini inapotokea mkeo akawa hayuko huru ni wakati wa kumuacha.
10. MPENDEZESHE MKEO AWE NA MUONEKANO MZURI.
Kadri mimba inavyokua basi mkeo huwa anapoteza uzuri mara nyingi atakonda au kama alikuwa mweupe atakuwa na weusi fulani. Kipindi hiki ni cha kuhakikisha matunzo yapo na mahitaji mengine.