MAKALA
Ajuza wa miaka 73 , Luisa Yu ameweka rekodi ya kutembelea nchi zote 193 Duniani ambao ni wanachama wa jumuiya ya umoja wa Mataifa (UN) ,jukumu ambalo amedumu nalo toka akiwa binti mdogo.
“Nilipokuwa naenda sinema, niliona mandhari nzuri kuhusu maeneo, asili,mito,milima, mabonde na hilo lilinivutia na kujiambia kuna siku nitasafiri na kujionea maeneo yote haya”.
Yu ambaye ni raia wa Ufilipino, amenukuliwa akisema alienda Marekani akiwa Mwanafunzi alipokuwa na umri wa miaka 23 na hapo ndio ukawa mwanzo wake wa kuanza kusafiri.
Kwa takribani miaka hamsini (50) , Bi Luisa amekuwa akisafiri kwenda popote alipotaka,kutoka katika nchi za Ulaya kama Italy hadi nchi za Asia kama Thailand 🇹🇭 na bara la Afrika hasa Libya na nchi za Mashariki ya kati kama Iran.