MICHEZO
Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) , Patrice Motsepe , ameipa maua yake Côte d’ivoire kwa maandalizi mazuri ya michuano ya Afrika ya mwaka huu na kuiita michuano ya kipekee.
Ameyasema hayo kwenye mkutano na Waandishi wa habari mjini Abidjan kabla ya mchezo wa fainali mnamo siku ya jumapili utakaoikutanisha Nigeria na mwenyeji Côte d’ivoire, Motsepe amesema karibu watu bilioni mbili Duniani wameyafatilia mashindano ya mwaka huu.
Mkuu wa idara ya mawasiliano ya CAF, Lux September amesema michuano hii inaelekea kuwa michuano “iliofanikiwa zaidi kibiashara “.
Kuhusu ishara walizoonyesha wachezaji wa DRC kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Afrika Kusini, Motsepe amesema
“Watu wa DRC wapo mioyoni mwetu na kuwa CAF ina jukumu kwa watu walioathirika na mizozo na migogoro.
Motsepe ametoa ahadi ya kuyatembelea maeneo yenye vita.