HABARI KUU
Rais wa Hungary amejiuzulu kutokana na ghadhabu ya raia baada ya kumsamehe mwanaume aliyekutwa na hatia katika kesi ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto.
Rais Katalin Novak alikuwa anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu kwasababu ya uamuzi wake wenye utata wa kumsamehe mwanaume ambaye alipatikana na hatia ya kufanya uhalifu wa kingono kwa watoto kwenye nyumba moja.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 46 ametangaza ujumbe huo kupitia Televisheni mnamo Jumamosi Februari 10,2024 kwamba amejiuzulu wadhifa wake wa urais ,baada ya kukaa madarakani toka 2022.
Novak alikuwa ni Rais mdogo zaidi kuwahi kuiongoza Jamhuri hiyo ya Hungary.