0:00
HABARI KUU
Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Edward Ngoyai Lowassa mwenye umri wa miaka 70 amefariki Dunia leo Februari 10,2024 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), jijini Dar es salaam.
Taarifa ya kifo cha kiongozi huyo wa zamani kimetangazwa leo na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango.
Edward Ngoyai Lowassa alikuwa Mwanasiasa wa muda mrefu akiwa pia amelitumikia jeshi la Tanzania na amekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kati ya mwaka 2005 mpaka 2008 alipojiuzulu nafasi hiyo kubwa ya kiserikali.
Bwana Lowassa alikuwa Waziri Mkuu kipindi cha awamu ya Nne chini ya Jakaya Kikwete ambapo baada ya kujiuzulu wadhifa wa Waziri Mkuu, Rais Jakaya Kikwete alimteua Mizengo Kayanza Peter Pinda kuchukuwa nafasi hiyo.
Related Posts 📫
Nigerian sensation Davido, also known as David Adeleke, has once...
Holders Manchester United will travel to record 14-times winners Arsenal...
In a press conference, Acting Inspector General of Police Douglas...
Olusegun Obasanjo, the former President of Nigeria, has paid a...
The Portugal midfielder has scored 79 goals and contributed 67...