MAPENZI
1. UJINGA .
Mahusiano huaribika haraka sana tofauti na yanavyojengwa kwa muda mrefu. Ujinga wa mtu ni kama ,kwa mwanaume kuona pesa inaweza kumpa Mwanamke yeyote na pia Mwanamke kuamini kuwa uzuri unaweza kumpatia mwanaume yeyote. Ujinga kwenye mahusiano ni kama kuamini unaweza kurusha yai juu na kutegemea kuwa litabaki salama.
2. MAMBO MAZURI YANAHITAJI JITIHADA NA MUDA.
Ili ujenge mahusiano mazuri ni lazima uwe na bidii na uwekeze kwenye muda na pia ili ubomoe mahusiano ni lazima upunguze jitihada na pia upuuze suala la muda.
3. NIA.
Ili uwe na mahusiano ya dhati lazima nia iwepo na pia ukikosa nia kwenye mahusiano basi ndio huwa chanzo cha ukomo wa mahusiano.
4. EPUKA MAWAZO YA WATU.
Mahusiano yako ni ya kipekee kwahiyo kuiga kwa namna yoyote ile namna wenzako wanavyofanya ni kuikosa thamani ya Mahusiano yako.
5. MAPENZI NI ZAIDI YA HISIA.
Mahusiano ni upendo unaotakiwa kujengwa kuanzia kwenye akili na sio kwenye moyo. Moyo umebeba hisia lakini akili imebeba upendo. Epuka sana kupenda kwa hisia maana hisia zina ukomo.
6. MAHUSIANO YANA MAJARIBU.
Unapopitiwa kwenye kipindi hiki sio muda wa kuachana bali ni moja ya hatua mtakuwa mmepiga. Majaribu huja na kuondoka, kuwa imata na mtangulize MUNGU mbele.
7. BUSARA.
Mapenzi hujengwa kwa jambo hili pia likiwepo na pia uvunjika kama busara itakosekana. Kwanini busara? Busara inakupa wewe kutotoa hukumu ambayo haistahili na pia inakupa muda wa kujihakikishia kama maamuzi utakayofanya yatakuwa ya msingi na sio ya kukurupuka.
8. MSAMAHA.
Hasira ya siku moja inaweza kubadilisha maisha yako yote,kwahiyo kabla ya Mambo yote jifunze kusamehe na kuruhusu upepo mpya kuingia.
9. MAJIVUNO.
Kiburi huwa kinapumbaza na kukuonyesha kuwa huko sahihi lakini ukiweka kiburi basi utaona mwenza wako nae sio mkamilifu kama wewe. Jifunze kusamehe na mfundishe mwenza wako kuwa bora kama unavyotaka.
10. HISIA.
Ni nzuri kwenye mahusiano lakini ziwe ni chanya lakini zikiwa hasi ndio huamasisha watu wengi kuwaka hasira. Hisia hasi zinaweza kukuharibia mahusiano uliyoyajenga kwa miaka mingi na kwa gharama kubwa ndani ya sekunde ya saa.