MICHEZO
Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakimsakama , Alex Iwobi (27) ,kwenye mitandao ya kijamii ,wakimlaumu kwasababu ya timu yao ya taifa kupoteza mchezo wa fainali dhidi ya mwenyeji Côte d’ivoire.
Alex Iwobi, ambaye alitolewa uwanjani dakika ya 79 na mchezaji mwenzake Alhassan Yusuf kuchukua nafasi yake.
Kutokana na mashambulio kwenye mitandao hiyo ya kijamii, Mchezaji huyo alilazimika kufuta picha zake zote kwenye mitandao yake ya kijamii mnamo siku ya Jumatatu Februari 12,2024.
Nahodha wa timu ya Taifa ya Nigeria 🇳🇬, Ahmed Musa na baadhi ya Wanigeria wamemtetea Iwobi na kusema sio haki kumlaumu mchezaji huyo pekee.
“Wapendwa mashabiki, naomba nitoe wito wa kuacha unyanyasaji wa kimtandao dhidi ya Alex Iwobi.
Kupoteza mchezo kweli ni jambo gumu ,lakini kumshambulia mchezaji mmoja pekee kwa jambo ambalo ni la timu nzima sio haki. Tunashinda kama timu na tunapoteza kama timu.Alex alijituma sana ,uwanjani kama mchezaji mwingine kwenye kikosi chetu”.
Mpaka sasa Alex Iwobi hajatoa tamko lolote kuhusu shutuma hizo.