MICHEZO
Kiungo wa England na timu ya Real Madrid ataukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya RB LEIPZIG kutokana na majeraha ya mguu.
Kiungo huyo fundi alitolewa nje ya uwanja huku akiwa amefunga mabao mawili dhidi ya Girona kwenye ushindi wa kalamu ya mabao 4-0 .
Naye Meneja wa timu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti amesema,
“Hatuna Bellingham, lakini bila yeye tumeshinda mechi nne,kati ya mechi nne . Majeraha haya yanakuwa fursa kwa wachezaji wengine. Tunaweza kufanya vizuri dhidi ya RB LEIPZIG.
Tupo kwenye mwendelezo mzuri ,tuna motisha ya kutosha kwenye mashindano tunayoyapenda sana”.
Pamoja na kauli hiyo ya ,Carlo Ancelotti ni kwamba haijafahamika kiungo huyo Muingereza atarejea lini uwanjani?
Magoli mawili aliyofunga yanafikisha jumla ya Magoli 20 kwenye michezo yake yote ya kimashindano 31 ndani ya Real Madrid.