MAMBO 10 YA KIMAPENZI YA KUFANYA SIKU YA VALENTINE KWA WANA NDOA

0:00

MAPENZI

Ikiwa leo ni siku ya Valentine basi kwa wana ndoa ni muda sahihi kuwa na ubunifu kwenye siku hii muhimu kwa mambo haya:-

1. KIFUNGUA KINYWA KITANDANI.

Kifungua kinywa kiwe cha mvuto kwaajili yenu kama wana ndoa na kiwe kitamu ambacho nyote mtakifungua mkiwa kitandani. Ubunifu kama huu utaichangamsha siku hii kwenu.

2. PIKA CHAKULA CHA USIKU WOTE.

Siku ya Valentine,wewe na mwenza wako ni vizuri kuingia jikoni wote na kusaidiana kupika chakula. Vaa mavazi rasmi ya jikoni na saidianeni kupika,hii urudisha hisia pia za kipindi cha uchumba.

3. MPE ZAWADI YA MAUA AU MAPULIZIO.

Huenda una mambo mengi ya kufanya, lakini kwa mwenza wako kumpa zawadi ya maua au mapulizio kwenye siku ya Valentine ni jambo la mvuto kimapenzi.

4. MPELEKE SEHEMU YA TOFAUTI.

Siku ya Valentine ni maalumu kwa wapendanao, mpeleke mwenza wako sehemu mpya ambayo hajawahi kufika au hamjawahi kufika. Ikiwezekana, iwe hotelini au maeneo kama ya starehe. Kufanya hivi utakuwa unaandika mwanzo mpya wa mapenzi.

5. TEMBELEA SEHEMU ZA MATUKIO.

Sehemu kama za Makumbusho , hoteli,bar huwa zinaandaa siku maalumu kwaajili ya Wapenzi. Maeneo kama haya utajiachia na mwenza wako na kusahau msongo wa maisha na kufungua mwanzo mpya wa Ndoa yenu.

6. TEMBELEA SEHEMU YA VICHEKESHO.

Hapa mnaweza kwenda kwenye ukumbi wenye wachekeshaji au kuangalia kwenye Televisheni vituko vya kuchekesha . Hii nayo ni jambo ambalo litaifanya siku ya Valentine kuwa ya kipekee.

7. TEMBELEA TAMASHA LA MUZIKI.

Hakuna raha kama kwenda na mpenzi wako kwenye Ukumbi wenye bendi ya muziki wa mubashara. Mke au Mume wako sehemu hii itampa raha na atajiona yuko kwenye mikono salama kwasababu ya kujaliwa.

8. PEANENI USIKU WA MAHABA.

Siku ya Valentine ni siku ya kupeana raha za maisha, ikiwezekana siku hiyo ,wewe na mwenza wako mtoke nje na maeneo mliyoyazoea. Mpeleke mwenza wako sehemu ambayo mnaweza kupeana hata chakula cha usiku.

9. MPE ZAWADI YA TOFAUTI.

Mnunulie simu,gari,nguo na zawadi ambayo kiukweli akiipata atajua umempa thamani yake kama mke au mume. Zawadi kwenye siku ya Valentine ni vizuri kutolewa kwa mbwembwe au kwa utofauti na siku zote.

10. TEMBELEA SEHEMU ZA WENYE UHITAJI.

Tembelea vituo vya watoto yatima au tembelea familia zinazoishi kwenye mazingira magumu. Wewe na mwenza wako, toeni misaada kama sehemu ya kutambua na kuthamini watu wote. Hii nayo ni ishara nzuri ya Upendo kwenye siku ya Valentine.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

See also  Real Madrid play their first home match of the 2024-25 season on Sunday, as they host Real Valladolid at the Santiago Bernabeu. Carlo Ancelotti’s side will be aiming to bounce back from last weekend’s disappointing opening weekend draw against Mallorca, and they are huge favourites to do so.

Related Posts 📫

Why Men are Important In a Marriage?
WHY MEN ARE IMPORTANT: Men are important in a marriage for...
Read more
It’s all about bouncing back without fear...
The world No. 13 pair brushed off their quarter-final exit...
Read more
WHY A CHEATING WOMAN IS MORE DANGEROUS...
A CHEATING WOMAN IS MORE DANGEROUS THAN POISON A man can...
Read more
Flick concerned by Barca's poor form without...
BARCELONA, - Barcelona's recent form is a major worry, manager...
Read more
WHAT WOMEN WANT AFTER SEX
When men want sex, they can say and do the...
Read more

Leave a Reply