MASTAA WA MAREKANI WANAVYOITUMIA SUPER BOWL KUKUA KIBIASHARA

0:00

MAKALA

Kampuni ya muziki ya APPLE huwa inatoa kiasi cha $50 million (bilioni 126 za Tsh) kwa ajili ya tamasha la muziki la Super Bowl kwa nusu muda.

Kiasi hicho cha pesa ,wasanii huwa hawachukui chochote mathalani mwaka huu tumemuona Usher Raymond.

Wengi wa wasanii hutumia jukwaa hili kuongeza Followers, kuuza tiketi na pia kuongeza streams kwenye mitandao yao.

ORODHA YA WASANII WALIOWAHI KUPANDA JUKWAA LA SUPER BOWL

1.Prince

2. Michael Jackson

3. Bruce Springsteen

4. Beyonce

5. Justin Timberlake

6. The Rolling stone

7. Rihanna

Kwa orodha yao hakuna msanii ambaye amewahi kulipwa. Na hii ikoje? NFL wamesaini mkataba wa udhamini wa TSH 126 Billion na kwenye mkataba huo ,msanii anatakiwa kulipwa zaidi ya bilioni 30 za Tanzania.

Kwenye bajeti hiyo,kuna watu kati ya 2,000 na 3,000 ambao wanahusika na masuala ya kupamba,kubuni,masoko nk hawa ndio uchukua kiasi hiki cha pesa na wakati mwingine msanii hulazimika kutoa pesa zake kuongeza kwenye bajeti hiyo. Mfano, The Weekend alitoa kiasi cha zaidi ya Tsh bilioni 3 kwenye Super Bowl ya 55 na inatajwa pia na Dr. Dre amewahi kutoa kiasi sawa na hicho.

KWANINI WASANII HUWA WANAYAFANYA HIVI NA ZIPI FAIDA?

Super Bowl inatazamwa na zaidi ya watu milioni 115 Duniani kote. Je ili sio zaidi ya jukwaa la kuonekana? Kwenye Super Bowl, Tangazo la sekunde 3 linalipiwa Tsh bilioni 3 huku msanii ambaye anaperfome kwenye jukwaa hilo akipewa dakika 13 ambazo hazina mwingiliano wa matangazo bure.

Kiukweli, hii ina thamani kuliko pesa ambazo angechukua.

FAIDA WALIZOPATA WASANII BAADA YA SUPER BOWL

1.Justin Timberlake mauzo ya muziki yalifikia 534% baada ya Super Bowl 52

2. Travis Scott kabla ya Super Bowl alikuwa analipwa bilioni 1 kwa show yake lakini baada ya Super Bowl 53 akaanza kulipwa bilioni 3 kwa kila show yake.

3. Jennifer Lopez na Shakira walipata followers milioni 3 baada ya Super Bowl ya 54.

4. Rihanna huyu ametisha sana . Baada ya Super Bowl amekuwa msanii namba moja mwenye streams nyingi Duniani, Nyimbo zake 17 zipo kwenye nyimbo 40 bora za Spotify, ameongeza followers milioni 3 Instagram na pia waliotafuta bidhaa zake za Fenty beauty wamefikia 833%

Huku pia waliomfatilia Rihanna wakifikia 118 na kuvuka wastani wa makadirio ya watazamaji wa Super Bowl.

Kwa mwaka huu,Usher Raymond ambaye ameachia album lake la “Coming Home” siku mbili kabla ya show yake kwenye jukwaa la Super Bowl anakwenda kuuza zaidi.

See also  KOCHA MIGUEL GAMONDI ATAJA ORODHA YA WACHEZAJI WATAKAOACHWA YOUNG AFRICANS

Baada ya performance yake Usher Raymond amesaini biashara nyingi za matangazo na huku pia akiuza tiketi hasa baada ya kutangaza atakuwa na tour ya miji 24 Duniani.

Sababu za wasanii kukubali kupanda kwenye jukwaa hili bure ni hiyo ya NFL ,kumpa Msanii dakika 13 za matangazo yake bure kwenye jukwaa linalotazamwa na watu milioni 115 na baada ya hapo msanii anakuwa habari nyingine kwa mafanikio.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

ARE YOU FIGHTING THE SYMPTOMS INSTEAD OF...
Many people in relationships and marriages are fighting symptoms and...
Read more
KURASA ZA MAGAZETI YA LEO YA TANZANIA
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
12 TRUTHS ABOUT BEING NAUGHTY
If you will not be naughty with your spouse, who...
Read more
HUYU NDIYE KOCHA WA SIMBA MPYA ...
MICHEZO ABDELHAK BENCHIKHA aliyewahi kuwa kocha mkuu wa USM...
Read more
Ivory Coast, Equatorial Guinea book Cup of...
CAPE TOWN, - Holders Ivory Coast and Equatorial Guinea became...
Read more

Leave a Reply