MANCHESTER UNITED YAWEKA REKODI YA KUWA KIKOSI GHALI ZAIDI DUNIANI

0

0:00

MICHEZO

Ripoti ya UEFA imesema kikosi cha Manchester United cha mwaka jana ndio cha gharama zaidi kuwahi kuundwa katika soka.

Taarifa ya taswira ya fedha na uwekezaji ya vilabu vya Ulaya imesema wachezaji wa Manchester United mwishoni mwa mwaka wa fedha 2023 waligharimu paundi bilioni 1.21 ,kwa kuchanganya na fedha za ada ya uamisho.

Mwaka 2020 kikosi cha Real Madrid ndio kilikuwa kikosi ghali zaidi Duniani kwa kiasi cha paundi bilioni 1.13.

Kikosi cha Manchester United kilijumuisha

1. ANTONY – Paundi milioni 82

2. HARRY MAGUIRE – paundi milioni 80

3. JADON SANCHO – paundi milioni 73

4. CASEMIRO- Paundi milioni 70

Jumla yake haijumuishi paundi milioni 72 za Rasmus Hojland ,paundi milioni 55 za Mason Mount na paundi milioni 47 za Andre Onana ,wote ambao walijiunga na Manchester United kwenye dirisha kubwa la usajili, kwenye majira ya joto 2023.

United ilimaliza katika nafasi ya tatu kwenye Ligi kuu ya England msimu uliopita,ikiwa ni msimu wa kwanza chini ya Meneja ,Eric Ten Hag.

Ripoti hiyo inasema vikosi vingine vitatu vya Manchester City, Chelsea na Real Madrid viligharimu paundi bilioni 1.

Takwimu za Chelsea ni za hadi mwezi juni 2022,ikimaanisha paundi milioni 850 walizotumia kwenye majira ya joto hadi Agosti 2023 hazijahesabiwa.

Mkataba wa Bilionea wa Uingereza, Sir Jim Ratcliffe wa kununua asilimia 25 ya hisa za Manchester United ulihidhinishwa na chama cha soka cha England FA siku ya jumatano.

Ununuzi huo una thamani ya takribani paundi bilioni 1.03 ,na kampuni yake ya Ineos Group itachukua udhibiti wa shughuli za soka.

Mujuni Henry
See also  WHY YOU ARE FRUSTRATING IN MARRIAGE
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading