MICHEZO
Yanga inaweza kuwa kwenye nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika endapo Al Ahly itaifunga CR BELOUZIDAD ya Algeria leo Februari 16,2024 .
Mchezo huo utapigwa kwenye ardhi ya Algeria mnamo saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki kwenye dimba la Julai 5.1962 jijini Algers, Algeria.
Ushindi wa Al Ahly kwenye mchezo huu utawafanya kusonga mbele kwa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Yanga nayo ikiwasubiri CR belouzidad ambapo ikifanikiwa kuwafunga basi nayo itakuwa imefuzu rasmi.
Yanga kwasasa ina alama 5 ambapo ikishinda mchezo wake na CR BELOUZIDAD basi itakuwa na alama 8 ambazo hakuna timu kwenye kundi hilo itazifikisha hata kama Yanga itadondosha alama dhidi ya Al Ahly kwenye mchezo wa mwisho utakaofanyika nchini Misri.
Matokeo ya leo, yakiinyima Al Ahly alama tatu basi itawapa Yanga wakati mgumu kwasababu watatakiwa kutafuta alama nne kwenye michezo miwili ya CR BELOUZIDAD na Al Ahly. Matokeo ya sare usiku wa leo yataifanya Al Ahly kuwa na alama 6,CR BELOUZIDAD 5 ambazo zitakuwa sawa na za Yanga.