MAMBO 20 YA KUZINGATIA KWA ALIYE NA AJIRA YEYOTEDiscoverCars.com

0:00

MASTORI

1. JENGA MAKAZI YAKO MAPEMA.

Iwe ni mjini au kijijini. Kujenga nyumba una miaka 50 hayo sio mafanikio. Usiruhusu hali ya kupendezwa na nyumba za serikali. Familia yako inapaswa kuishi kwenye nyumba yako na kustarehe.

2. UWE UNARUDI NYUMBANI.

Usipende kukaa kazini au kwenye majukumu yako. Wewe sio nguzo kwenye hiyo idara. Ukifa leo,hiyo nafasi atapewa mwingine na kazi zitaendelea kama kawaida. Familia kwako iwe kipaumbele.

3. USIKATAE FURSA.

Wekeza kwa kile unachofahamu na noa ujuzi wako ili uwe mahiri hata ikitokea ukapata nafasi kubwa basi uwe mbobevu.

4. EPUKA MAJUNGU YA KAZINI.

Majungu kwenye eneo la kazi ni jambo ambalo linaweza kupunguza hadhi yako hasa ilitokea ukawa na makundi ndani ya ofisi yako.

5. USISHINDANE NA WAKUBWA WAKO KAZINI.

Kufanya hivyo ni kujiunguza mikono na kushindana na marafiki zako ni kuumiza akili yako.

6. WEKEZA.

Mshahara hauwezi kutosha kwaajili ya mahitaji yako na familia yako.

7. WEKA AKIBA YA PESA.

Kila unachovuna ukikitumia chote basi kuna uwezekano wa kuwa mtumwa wa maisha.

8. KOPA KWAAJILI YA MAENDELEO NA SIO KUNUNUA VITU VYA ANASA .

Nunua au fanya anasa kwa faida utakazopata .

9. WEKA UFARAGHA WA MAISHA NDOA NA FAMILIA YAKO .

Mambo yote ya faragha yaweke mbali na kazi yako. Ni jambo la muhimu sana.

10. KUWA MWAMINIFU KWAAJILI YAKO MWENYEWE NA KAZI YAKO.

Ujiamini kwa kazi yako unayoifanya na usipende kujenga ukaribu na mkubwa wako kazini(uchawa), kwasababu kufanya hivyo ipo siku anaweza kukuachisha kazi.

11. PUMZIKA MAPEMA.

Siku ya kujiandaa kuacha kazi ni siku ile unapopokea barua ya kukubaliwa kwenye hiyo kazi. Siku ya kuacha kazi ni leo. Kwenye miaka 40 au 50 ni muda wa kupumzika.

12. IPENDE KAZI YAKO.

Kufanya kazi unayoipenda huleta matokeo chanya.

13. TUMIA MUDA WA RIKIZO VIZURI KWAAJILI YA MAENDELEO YAKO.

Muda wa kujenga mambo yako ni kipindi cha rikizo lakini kutumia rikizo kula bata ,usitegemes maajabu ukishastaafu.

14. BUNI MIRADI YAKO UKIWA KAZINI.

Muda mzuri wa kuweka miradi ni pale unapokuwa kazini na hakikisha miradi au mradi unaoanzisha unafanya vizuri na ukiwa na uhakika mradi wako unafanya vizuri basi fanya uamuzi uachane na hiyo kazi. Watu wengi huwa wanaanzisha miradi wakiwa wastaafu na uja kuambulia tu hasara.

15. KIINUA MGONGO SIO HELA YA KUFUNGULIA BIASHARA AU KUJENGEA NYUMBA BALI NI FEDHA YA KUKUTUNZA KUMALIZIA MAISHA YAKO UKIWA NA AFYA NJEMA.

Kiinua mgongo au hela ya mafao sio hela ya kuolea mke au kulipa ada za shule bali zipo kwaajili ya kukutunza wewe.

16. WEKA AKILINI,KWAMBA KUSTAAFU SIO SEHEMU YA KWENDA KWENYE MAJUTO BALI NI KUWA CHACHU YA KUWAFANYA WENGINE KUSTAAFU.

17.USISTAAFU KWASABABU UMEKUWA KAMA MZIGO KAZINI.

Unatakiwa kustaafu ukiwa sio mzigo bali mwenye nguvu za kuendelea kula maisha yako,kupokea hela zako ambazo umewekeza kwenye miradi mbalimbali. Wengi ambao huwa wanastaafu wakiwa mizigo huwa wanatumia muda mwingi kuendelea kufanya kazi badala ya kutumia muda huo kuwa karibu na familia zao na wakikosa hizo kazi huwa wanakufa mapema.

18. NI VIZURI KUSTAAFU UKIWA KWAKO KULIKO UKIWA KWENYE NYUMBA ZA SERIKALI KWANI UTAKUWA KARIBU NA JAMII ILIOKUKUZA NA KUKULEA.

Ni jambo gumu kuishi vizuri na jamii ambayo ulijitenga nayo kwa muda mrefu kwa kuishi kwenye nyumba za Kampuni au Serikali.

19. MARUPURUPU YA AJIRA YASIKUFANYE KUSAHAU KUWA KUNA KUSTAAFU.

Ajira isikufanye kula tu bata na kuamini kuwa hakuna maisha baada ya kustaafu . Kumbuka hakuna atakayekuita boss ukiwa umestaafu .

20. USICHUKIE KUSTAAFU KWASABABU IPO SIKU UTASTAAFU KWA HIARI AU KULAZIMISHWA.

Usichukie na kujiona mnyonge kwasababu ya kustaafu maana hilo ni suala la wakati.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

See also  Christiana Ashiaku scores hat-trick as Ghana thump Cote d'Ivoire in semis

Related Posts 📫

Arsenal have re-entered the race to sign...
Osimhen is widely expected to leave Napoli this summer, having...
Read more
Odinga Denies Bribery Allegations, Reaffirms Solidarity with...
Azimio la Umoja - One Kenya Coalition principal Raila Odinga...
Read more
A lady using new technology is perfect...
Nulla malesuada pellentesque elit eget gravida cum sociis natoque....
Read more
MAKONDA AGEUKIA DAWA ZA KULEVYA
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
KURASA ZA MAGAZETI YA HIVI LEO 25/06/2024
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more

Leave a Reply