MICHEZO
Shirikisho la soka Nchini Ivory limemteua Emerse Faé kuwa Kocha Mkuu wa kudumu wa timu ya Taifa hilo kufuatia mwenendo mzuri wa ‘The Elephants’ kwenye AFCON 2023.
Faé aliteuliwa kuwa Kocha wa muda wa Ivory Coast baada ya Mfaransa Jean-Louis Gasset (70) kutupiwa virago kufuatia mwanzo mbaya kwenye AFCON 2023 uliopelekea Ivory Coast kufuzu hatua ya 16 bora kama ‘best looser’.
Faé aliiongoza Ivory Coast kushinda mechi zote kuanzia hatua ya 16 bora, robo fainali, nusu fainali na fainali na kutwaa ubingwa wa AFCON 2023 kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Nigeria.