KATIBU MKUU CCM NCHIMBI AWATISHA VIONGOZI WAZEMBE

0:00

HABARI KUU

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, amewatahadharisha viongozi wote wanaotokana na CCM wasiotimiza wajibu wao kuwatumikia watu, kwa kadri ya matarajio ya Chama na wananchi, na badala yake wanatanguliza maslahi yao binafsi, siku zao zinahesabika, kwani CCM haiwezi kuwavumilia.

Dk. Nchimbi amesema kuwa viongozi wote wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi wanatarajiwa kuwa watumishi wa wananchi waliowachagua, wakiwatumikia kwa nguvu zao zote, wakiweka maslahi ya umma na Watanzania mbele wakati wote, kabla ya masuala yao binafsi.

Katibu Mkuu Dk. Nchimbi amesema hayo alipokuwa akisisitiza namna bora ya kumuenzi Hayati Balozi (mst) Deodorus Buberwa Kamala, kupitia salaam za pole na rambirambi za CCM wakati wa shughuli ya kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa marehemu, iliyofanyika leo Februari 20, 2024, kijijini kwao Rwamashonga, Kata ya Bwanjai, Jimbo la Nkege, Wilaya ya Misenyi, mkoani Kagera.

Mbali ya kutoa salaam za Chama Cha Mapinduzi, Balozi Dk. Nchimbi pia aliwasilisha salaam maalum za rambirambi kwa wafiwa na waombolezaji wote na kisha mkono wa pole kwa Familia ya Hayati Dk. Kamala, kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambapo pia alieleza jinsi Rais Dkt. Samia alivyoguswa na msiba huo.

Balozi Dk. Nchimbi ameongeza kusema kuwa mojawapo ya uwezo mkubwa wa kiuongozi aliokuwa nao Hayati Dk. Kamala ni pamoja na saikolojia ya kutafuta suluhisho la changamoto za watu, tangu alipokuwa Rais wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe, huku akimwelezea jinsi alivyokuwa muadilifu, aliyechukia rushwa kwa vitendo, kiasi cha kuwa tayari kugharimu na kupoteza Ubunge wa Jimbo la Nkenge, katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010, kwa sababu ya hakuwa tayari kupokea fedha kuwasaliti wananchi wa jimbo hilo, aliokuwa anawatetea kwenye changamoto zao.

“Kamala hakuwa mla rushwa. Hili naweza kulisemea kwa kiapo. Hata alipopoteza ubunge, hakuwahi kulalamika. Kwa sababu alijua zile zilikuwa ni hela za udhalimu, hela za usaliti kwa wananchi wake. Watu wa namna hii lazima tuwaenzi vizuri kwa kutambua mchango wao mkubwa”

See also  Tume ya Haki Za Binadamu Yamsafirisha PAULINE GEKUL Dhidi ya Udhalilishaji

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Kwanini Kauli ya Nape Nnauye Imepigwa na...
Kauli ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia na Teknolojia...
Read more
BUSINESS MARKETING RESEARCH
What Is Market Research? The term market research refers to the...
Read more
President Ruto Challenges Gen Z Protesters to...
In a speech delivered in Taita Taveta, President William Ruto...
Read more
PAPA ASHINDWA KUJIBU SWALI KUHUSU JAMII YA...
HABARI KUU. Watu waliobadili jinsia wanaweza kuwa wazazi wa ubatizo...
Read more
PRINCE DUBE NA AZAM FC KIMEELEWEKA
MICHEZO Klabu ya Azam FC imeshinda kesi dhidi ya mshambuliaji...
Read more

Leave a Reply