HABARI KUU
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesema nchi haina uhaba wa dola, bali baadhi ya watu wamezihifadhi wakitarajia bei itapanda, ikisisitiza hakutakuwa na ongezeko hilo kutokana na hatua za ndani na nje zinazochukuliwa katika kuimarisha upatikanaji wake.
BoT imezitaja hatua hizo ambazo ni pamoja na uamuzi wa Marekani kulegeza masharti ya riba kwenye masoko yake ya fedha, kupungua kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia na ya nchini na kuendelea kutoa bei elekezi na kufuatilia kwa karibu sekta ya fedha nchini.
Meneja Msaidizi Utafiti wa BoT, Dk. Lusajo Mwankemwa, amebainisha hayo alipotoa mada kuhusu majukumu ya taasisi hiyo benki hiyo wakati wa semina kwa waandishi wa habari, ambao walitaka kujua hatua zinazochukuliwa kuimarisha upatikanaji dola nchini.
“BoT tunajua na tunaona dola zipo ila ni ngumu kukufuata kutaka tuchukue dola nyumbani kwako, mimi (BoT) nitasema dola moja ni kiasi hiki (bei elekezi).