MICHEZO
Nyota wa muziki wa Afrobeat kutoka Nigeria, Davido ametangaza kuwa atachangia Naira milioni 300 (shilingi milioni 500) kwenye vituo vya watoto yatima nchini humo.
Davido, ambaye jina lake halisi ni David Adeleke, kwa miaka ya karibuni amekuwa akito misaada kwa jamii ambapo mwaka 2021 aligawa Naira milioni 250 (takribani shilingi milioni 320) kwa vituo vya watoto yatima. Hii ilikuwa ni baada ya mashabiki kumchangia Naira milioni 200, na yeye kuongezea Naira milioni 50.
Alichangiwa fedha hizo baada ya kuchapisha ujumbe kwenye mtandao wa X, wakati huo Twitter, akiwaomba mashabiki wamchangie fedha akomboe gari lake, Rolls Royce, kutoka bandarini.
Baada ya hapo alianzisha taasisi ya David Adeleke ambayo imekuwa ikitoa fedha kwa vituo vya watoto yatima.