WAASI WA CONGO WAWEKEWA VIKWAZO NA UMOJA WA MATAIFA

0:00

HABARI KUU

Umoja wa Mataifa umeweka vikwazo vya usafiri, silaha na kupiga tanji amana za viongozi sita wa makundi ya waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, huku ghasia zikizidi kurindima mashariki mwa nchi hiyo.

Waliowekewa vikwazo ni pamoja na msemaji wa kundi la waasi la M23, Jenerali wa kundi la FDLR, na viongozi wawili wa kundi la ADF.

Wengine ni kiongozi wa kundi la Mai-Mai la CNPSC na kamanda wa kundi la Twirwaneho.

Tangazo hili limekuja kufuatia mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne, uliolenga kujadili hali tete ya DRC.

“Tunatangaza kuanzia leo, viongozi wengine sita wa makundi ya watu wenye silaha watawekewa vikwazo,” amesema Robert Wood, mwakilishi wa Marekani wa masuala ya siasa kwenye Umoja wa Mataifa.

“Watu hawa wanahusika na matukio mengi ya unyanyasaji,” amesema.

Makundi ya M23 na FDLR yamekuwa katikati ya mvutano kati ya serikali za DRC na Rwanda.

DRC inaituhumu Rwanda kwa kuunga mkono kundi la M23 huku Rwanda ikilaumu jirani yake kwa kushirikiana na kundi la FDLR, ambalo Rwanda inasema wanahusika na mauaji ya Kimbari ya 1994.

Kwenye kikao cha Jumanne cha Baraza la Usalama, wajumbe walilaani kusonga mbele kwa kundi la M23 kuelekea mji wa Sake, jambo ambalo limesababisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao.


Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Murulle Youth Emphasize Family Unity at Nairobi...
Learnered youth from the Murulle community, particularly from the Ali...
Read more
Poison that kills a man.
Once upon a time a beautiful girl got tired of...
Read more
Neymar returns to Al-Hilal training after injury...
Neymar took part in team training and will join the...
Read more
Benjamin Mendy wins most of $14 mln...
LONDON, - Former Manchester City defender Benjamin Mendy won a...
Read more
HOW TO TOUCH A WOMAN
LOVE TIPS ❤
See also  MAPIGO 10 YA CCM KWA MZEE EDWARD LOWASSA ALIYOPITIA BAADA YA KUJIUNGA NA CHADEMA
A woman loves to be touched by...
Read more

Leave a Reply