DANI ALVES AHUKUMIWA KIFUNGO JELA

0:00

MICHEZO

NYOTA wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil, Dani Alves amehukumiwa kifungo cha miaka minne na miezi 6 jela baada ya kukutwa na hatia ya kumnyanyasa kingono mwanamke mmoja katika klabu ya usiku ya Barcelona mnamo mwaka 2022.

Uamuzi huo umefanywa na Mahakama kuu Nchini Uhispania ambayo sambamba adhabu hiyo imemuamuru beki huyo wa zamani wa Barcelona alipe euro 150,000 kwa mwathirika.

Alves (40) alikuwa ameshikilia kuwa ngono hiyo ilikuwa ya makubaliano. Mwendesha mashtaka alikuwa akitaka kifungo cha miaka tisa jela.

Hii ni mojawapo ya kesi zenye hadhi ya juu zaidi nchini Uhispania tangu sheria iliyopitishwa mwaka wa 2022 kufanya idhini kuwa kipengele muhimu katika kesi za unyanyasaji wa kijinsia na kuongeza muda wa chini wa jela kwa mashambulizi yanayohusisha unyanyasaji.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

HENDERSON MBIONI KUREJEA ULAYA
MICHEZO Klabu ya Juventus ya Italia imeripotiwa kufanya mazungumzo na...
Read more
FRANK LAMPARD WANTS COLE PALMER TO BECOME...
SPORTS Legendary footballer and former Chelsea manager Frank Lampard has...
Read more
LHRC KUMSHITAKI OSCAR OSCAR
NYOTA WETU Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)...
Read more
CARLO ANCELOTTI MATATANI KWA UKWEPAJI KODI ...
NYOTA WETU Meneja wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti...
Read more
HATIMAYE AMETOKA HOSPITALINI BAADA YA KULAZWA KWA...
Mtoto Maliki Hashimu, mkazi wa Goba Jijini Dar es Salaam,...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Lord's Chosen Reacts To 'AK-47' Testimony

Leave a Reply