MICHEZO
Klabu ya Yanga imeingia Mkataba wenye thamani ya Tsh milioni 300 na kampuni ya usafirishaji ya Karimjee Group inayotengeneza pikipiki za Hero Duniani utakaodumu kwa kipindi cha miezi 18.
“Leo tumeingia makubaliano na kampuni ya Karimjee Mobility kupitia kampuni ya Hero ambayo inatengeneza pikipiki na kusambaza. Kampuni ya Hero inatajwa kuwa kampuni namba 1 duniani kwa biashara hiyo”. —Rais wa Young Africans SC Eng. Hersi Said
Kampuni hii kutoka India inafanya biashara mataifa zaidi ya 40. Young Africans SC itapata kiasi cha Tsh Milioni 300 kutoka kwenye mkataba huu katika kipindi cha miezi 18″—Eng. Hersi Said
Kwa upande wake Mkuu wa Masoko kutoka Karimjee Group, Nada Vievi, amesema pikipiki hizo zitakuja na Bima kwa mteja pamoja na kofla mbili zenye nembo za Yanga.