MICHEZO
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi ametangaza kumpatia zawadi mchezaji Luvumbu Nzinga ambaye ameachana na klabu ya Rayon Sports ya Rwanda hivi karibuni.
Katika mkutano na waandishi wa habari alifahamisha kuwa Luvubu alionyesha ushujaa katika kuwapigania wananchi wa DRC waliopo Kaskazini mwa nchini hiyo ambao wanaendelea kuyakimbia makazi yao kutokana na mapigano yanayowahusisha jeshi la nchi na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda.
Pia aliweka wazi kuzungumza na Mwenyekiti wa timu ya AS Vita Club na kukubali kumsaini mchezaji huyo baada ya kuachana na Rayon Sports.
Hivi karibuni ushangiliaji wake ulizua mjadala nchini Rwanda na kupelekea Shirikisho la soka Rwanda FERWAFA, kumsimamisha miezi sita kujihusisha na soka kwa madai ya kuchanganya soka na siasa.