SAKILU AVUNJA REKODI YA MTANZANIA

0:00

MICHEZO

Mwanariadha wa Tanzania Jackline Sakilu ameshika nafasi ya tatu katika mbio za nusu marathoni za Ras Al
Khaimah zilizofanyika leo Februari 24, 2024 huko Falme za Kiarabu na kuvunja rekodi iliyowekwa na mwenzake, Magdalena Shauri miaka minne iliyopita.

Katika mbio hizo Sakilu alikimbia kwa muda wa 1:06:04 ambao umemfanya aweke rekodi ya taifa na kuvunja ile iliyowahi kuwekwa na Magdalena Shauri mwaka 2020 ya kukimbia kwa muda wa 01:06:37 katika mbio hizohizo za Ras Al Khaimah.

Mshindi wa kwanza katika mbio hizo ni Tsigie Gebreselama wa Ethiopia akitumia muda wa 01:05:14, huku mshindi wa pili akiwa Muethiopia mwenzake, Ababel Yeshaneh.

Wakenya wanne wameshindwa kufua dafu mbele ya Sakilu ambao ni Margaret Chelimo aliyekamata nafasi ya nne, Evaline Chirchir nafasi ya tano, Catherine Amanangole nafasi ya sita na Peres Jepchirchir aliyekamata nafasi ya saba.

Kwa kuibuka mshindi wa tatu kwenye mbio hizo, Sakilu amejihakikishia kupata Dola 7,000 za Marekani (Sh 17.8 milioni) wakati mshindi wa kwanza akipata Dola 15,000 na wa pili akipata Dola 10,000.

Kwa upande wa wanaume, nafasi tatu za juu tofauti zimekamatwa na Wakenya, Daniel Kibet Mateiko aliyeibuka mshindi, akifuatiwa na John Korir na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Isaia Lasoi huku Mtanzania Felix Simba akishika nafasi ya 10.

Hata hivyo Simbu hajaondoka mikono mitupu kwani amepata kiasi cha Dola 1000 (Sh 2.5 milioni) kwa kumaliza katika nafasi hiyo ya 10.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

BITEKO AANIKA KIINI CHA KUKATIKA UMEME NCHINI...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
ONYO KWA WATUMIAJI WA NGUVU ZA KIUME...
MAGAZETI
See also  Bola Tinubu of the ruling party has removed Solomon Arase from his position as Police Commission Chairman and named a replacement.
Karibu Mtanzania kwenye magazeti ya leo kwenye mbao za...
Read more
SKILLS EVERY PROFESSIONAL SHOULD LEARN IN LIFE
Communication skills: Effective communication is essential in any professional setting....
Read more
BONDIA MTANZANIA DULLA MBABE APIGWA KWA KNOCK...
MICHEZO Bondia Mtanzania Abdallah Pazi almaarufu Dulla MBABE amepigwa kwa...
Read more
HOW TO GROW CARROTS
Choose the right location: Carrots prefer full sun and well-drained...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply