MUHIMBILI-MLOGANZILA YAINGIZA BILIONI 8 KISA UREMBO

0:00

HABARI KUU

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imezalisha shilingi Bilioni 8 kwa kufanya tiba urembo ambapo pia wameboresha maeneo mengi ya huduma ikiwemo ununuzi wa vifaa bora na vya kisasa na kuboresha chumba cha kuhifadhia maiti.

Amesema hayo wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI ambayo imeeleza kuridhishwa na hali ya utoaji huduma katika hospitali hiyo.

“Niipongeze Serikali kwa kuboresha huduma za afya nchini kwani hivi sasa asilimia 90 ya wagonjwa ambao walikuwa wanakwenda nje ya nchi kutibiwa wanatibiwa hapa nchini na tumeanza kupata wageni kutoka nje ya nchi kuja kupata huduma nchini,” ameeleza Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Faustine Ndugulile.

Aidha, ameitaka Serikali kupanua wigo wa utoaji huduma katika hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwani hospitali hiyo bado ina eneo kubwa.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

WILL SMITH NDOA YAKE IMEMSHINDA ...
NYOTA WETU Muigizaji na mtangazaji Jada Pinkett Smith ameweka wazi kuwa...
Read more
AL AHLY YAONDOLEWA KLABU BINGWA YA DUNIA
MICHEZO Mabingwa wa Afrika, AL AHLY wametolewa kwenye michuano...
Read more
President Ruto Nominates Dorcas Oduor as Kenya's...
President William Ruto has nominated Dorcas Oduor to serve as...
Read more
YANGA YAINGIZA PESA NDEFU KWENYE TAMASHA LAKE...
Dar es salaam. Matamasha ya Wiki ya Mwananchi na Simba...
Read more
Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson amempa...
Mvutano mkali umeibuka bungeni leo Juni 4, 2025 kati ya...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  TLS Yaanika Wazi Orodha Ya Waliotekwa na Kupotezwa

Leave a Reply