0:00
MICHEZO
Adhabu ya klabu ya Everton ya kupokonywa pointi kumi kwa kukiuka sheria za fedha za Ligi Kuu ya England, imepunguzwa hadi pointi sita, baada ya kukata rufaa.
Everton ilinyang’anywa pointi 10 mwezi Novemba kwa kuvunja sheria ya faida na uendelevu (PSR) katika kipindi cha miaka mitatu.
Adhabu hiyo- ambayo ni kubwa kuwahi kutolewa kwenye EPL- iliidondosha Everton kutoka nafasi ya 14 hadi 19 kwenye msimamo wa ligi.
Kupunguzwa kwa adhabu hiyo kunawainua Everton kutoka nafasi ya 17 hadi 15, ingawa klabu hiyo inakabiliwa na uwezekano wa adhabu nyingine ya kupokonywa pointi zake.
Everton ambao walikiri kuvunja sheria wamesema “wameridhishwa” na kupunguziwa adhabu.
Related Posts 📫
HARD NEWS
Three of the Chibok girls who fled from...
Michezo
USM Alger imetwaa taji la CAF Super Cup ikiwachapa...
The Saints will pay an initial £18m for the former...
CELEBRITIES
Nigerian singer, Spyro opens up about his deep admiration...