MAZISHI YA KIHISTORIA YA RAIS HAGE GEINGOB

0:00

HABARI KUU

Hatimaye aliyekuwa rais wa Namibia, Hage Geingob ambaye alifariki akiwa hospitali Februari 4, 2024 wiki kadhaa baada ya kupatikana na saratani, amezikwa kwenye bustani ya mashujaa ya Heroes Acre, hapo jana siku ya Jumapili Februari 25, 2024.

Mazishi hayo yalifanyika katika viungani vya mji mkuu wa Namibia Windhoek, baada ya siku 20 za maombolezo, huku wanajeshi wakifyatua mizinga 21 kwa heshima, wakati ndege za kivita za kijeshi zikipaa angani kwenye eneo hilo.

Geingop (82), aliwahi kuwa Waziri Mkuu mara mbili na baadaye kuwa rais wa 3 wa Taifa hilo tangu lilipojipatia uhuru wake kutoka Afrika Kusini 1990, akiongoza nchi hiyo yenye watu wachache na sehemu kubwa ikiwq ni jangwa, kuanzia mwqka 2015.

Kama mmojawapo wa Wanaharakati wa uhuru, Geingop alikimbilia kwenye mataifa ya kigeni kwa miaka 27, yakiwemo Botswana, Zambia na Marekani, kabla ya kurejea nchini 1989 na aliwahi kuhudumu kwenye nyadhifa mbalimbali serikalini na chama tawala cha South West African People’s Organisation – SWAPO.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MASHABIKI ARSENAL KUMSAJILI DECLAN RICE ...
MICHEZO. Kundi la mashabiki wa Arsenal wameanzisha ukurasa maalamu wenye...
Read more
TAARIFA YA PACOME ZOUZOUA KWA SASA
MICHEZO Kiungo wa klabu ya Yanga, Pacome Zouzoua ambaye alipata...
Read more
5 THINGS MEN WANT FROM WOMEN IN...
LOVE TIPS ❤ DEAR LADIES 1) PEACEOne of the greatest...
Read more
Real Madrid play their first home match...
Valladolid will arrive in the Spanish capital with confidence, having...
Read more
Diddy’s kids celebrate his birthday with heartfelt...
In a heartfelt display of familial love, Sean 'Diddy' Combs...
Read more
See also  NAULI ZA TRENI ZA TRC HIZI HAPA

Leave a Reply