HABARI KUU
Rais Joe Biden amewaasa wasaidizi wake kwamba siri ya ndoa ndefu na ya kudumu ni “tendo la ndoa,”
–
Kwa mujibu wa kitabu kipya kuhusu mke wa rais Jill Biden ambacho kinaangazia ndoa yao iliyodumu kwa miaka 47 sasa, ‘Tendo la ndoa’ ndio kirutubisho muhimu zaidi.
–
Kitabu hicho “American Woman – The Transformation of the Modern First Lady, from Hillary Clinton to Jill Biden,” kimeandikwa na mwandishi wa New York Times katika ikulu ya White House Katie Rogers na kinatoka wiki hii.
–
Sehemu inayohusu ngono inachukua vifungu vichache tu katika kitabu hicho chenye kurasa 276 lakini tayari kimeibua mjadala mkubwa mitandaoni na kugonga vichwa vya habari kote duniani.
–
Jill Tracy Jacobs Biden, mke wa pili na wa sasa wa Biden, alizaliwa Juni 3, 1951. Alikutana na Biden Machi 1975.
–
Kitabu hiki kinaelezea uchungu wa Biden baada ya mke wake wa kwanza, Neilia, kufariki katika ajali ya gari mwaka wa 1972 pamoja na binti yao Naomi.
–