MICHEZO
Mshambuliaji wa Man Utd, Anthony Martial ataondoka kwenye kikosi hicho katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ambapo mkataba wake utamalizika na Man United imekataa kutumia kipengele cha kuurefusha mkataba huo kwa mwaka mmoja zaidi.
Martial mwenye umri wa miaka 28, alidaiwa kuwa angeondoka tangu Januari mwaka huu ambapo Marseille, Fernebanhce na timu kibao kutoka Saudi Arabia zilidaiwa kuwa tayari kumsajili.
Kocha wa Man United, Erik ten Hag haonekani kuvutiwa na kiwango cha staa huyo na ameripotiwa kuwasilisha pendekezo la kusajiliwa straika mwingine dirisha lijalo.
Martial ni mmoja kati ya mastaa wanaochukua pesa nyingi kwenye kikosi cha Mashetani Wekundu na mbali ya kwamba Ten Hag havutiwi na kiwango chake, pia imewahi kuripotiwa mara kadhaa kwamba tajiri mpya Sir Jim Ratclife anahitaji kuondoa baadhi ya mastaa ili kusuka upya kikosi kwa ajili ya msimu ujao.