HABARI KUU
Rais wa Marekani Joe Biden amesema anatumai kuwa hadi Jumatatu ya wiki ijayo vita ya Israeli katika Ukanda wa Gaza itakua imesitishwa.
“Kwa hakika natarajia kufikia mwanzoni mwa mwisho wa wiki hii angalau……….. kwa jinsi ninavyoambiwa na mshauri wangu wa masuala ya usalama ni kwamba tupo karibu, tupo karibu lakini bado, matarajio yangu ni kwamba kufikia Jumatatu ijayo tutakuwa na usitishaji wa mapigano” ——— Rais Biden.
Imeelezwa kwamba katika majadiliano ya kusitisha mapigano hayo huko Doha, Qatar Wajumbe kutoka Hamas na Israel walifanya mazungumzo kwa nyakati tafauti jana Jumatatu ambapo upande wa Israel ulisema ikiwa awamu mpya ya usitishaji mapigano itakubaliwa, watakubali kusitisha mapigano ili kuhakikisha mateka wanaachiliwa lakini operesheni yake ya jeshi la ardhini itaendelea.
Wakati hayo yakisemwa na Israel, upande wa Hamas ulisisitiza kuwa usitishaji wa kudumu wa mapigano ndilo hakikisho pekee la kufikiwa kwa makubaliano hayo.