MICHEZO
Meneja wa Chelsea Mauricio Pochettino amesema wamiliki wa klabu hiyo wameonesha kumuunga mkono tangu alipopoteza mchezo wa fainali ya Carabao dhidi ya Liverpool.
Pochettino alishutumiwa na mashabiki na hata wachambuzi baada ya Chelsea kufungwa 1-0 na Liverpool dhaifu siku ya Jumapili.
Alisema amekuwa na mazungumzo chanya na wamiliki Todd Boehly na Behdad Eghbali.
“Wameonesha kuniunga mkono na baada ya mchezo Todd alinitumia ujumbe mzuri tu,” alisema Pochettino.
“Nilisalimiana nao nilipowaona uwanjani na baadaye nilikutana na Behdad na tukazungumza.
“Tulizungumza kuhusu mchezo na nafasi tuliyopoteza ya kushinda kombe, kwa sababu nadhani tulicheza vizuri katika dakika 90.”
Alipoulizwa kuhusu hatma yake Chelsea, Pochettino alisema: “Sio juu yangu. Tuna uhusiano mzuri sana na wamiliki na mkurugenzi wa michezo.
“Ni juu yao kuniamini au kutoniamini. Sio uamuzi wa kocha.”