MICHEZO
Msanii kiongozi wa Kundi la Reggae la Morgan Heritage, Peter “Peetah” Morgan, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 46.
Taarifa za kifo chake zilitangazwa jana, Februari 25, 2024 na bendi hiyo pamoja na familia yake ambayo imeomba faragha katika kipindi hiki cha maombolezo.
Licha ya familia ya Morgan kutoeleza chanzo cha kifo cha msanii huyo, mwandishi wa habari na mdau mkubwa wa muziki nchini Jamaica, Sean ‘Contractor’ Edwards, ameliambia Jarida la DancehallMag kwamba Morgan alifariki nchini Marekani baada ya kupatwa na kiharusi.
“Bila shaka, ugonjwa ni suala la faragha sana, na ni daktari tu anayeweza kutoa maoni sahihi juu ya sababu halisi ya kifo, lakini nilichojua ni kwamba alipatwa na kiharusi na kufariki Marekani,” alisema.