HABARI KUU
Rais wa Algeria Abdelmajid Tebbourne siku ya Jumapili alizindua Msikiti Mkuu wa Algiers, ambao ni msikiti mkubwa zaidi barani Afrika.
Msikiti huu ni wa tatu kwa ukubwa duniani, nyuma ya misikiti miwili iliyopo Maka na Madina.
Msikiti huo umejengwa katika eneo lenye ukubwa wa hekari 70 na unaweza kuchukua waumini 120,000.
Msikiti huu pia una mnara mrefu zaidi duniani.
Unatarajiwa kutumiwa wakati wa mwezi wa Ramadhan unaoanza wiki mbili zijazo.
Msikiti huu ulijengwa kwa muda wa miaka saba na kugharimu zaidi ya dola milioni 800.
Ujenzi wa msikiti huu ulikuwa mradi wa Rais wa zamani wa Algeria Abdelaziz Bouteflika ambaye aliondoka madarakani baada ya nia yake ya kutaka kuwania urais kwa muhula wa tano kusababisha maandamano makubwa.