HABARI KUU
Mwili wa Mtanzania Abraham Mgowano aliyekuwa akiishi na kufanya kazi katika Kampuni ya Google kama Mhandisi wa Programu Endeshi (Software Engineer) umepatikana ukielea katika Mto Miami jijini Florida baada ya kuanguka toka kwenye Boti (Yacht)
Abraham aliripotiwa kupata ajali Februari 24, 2024 akiwa na wenzake 12 pamoja na Kapteni wa Boti hiyo. Polisi walianza kumtafuta kwa kutumia Boti nyingine na Helikopta bila mafanikio hadi walipopata taarifa za kupatikana kwa mwili huo ukielea Februari 27, 2024
Kwa mujibu wa taarifa, Abraham alikuwa Mfanyakazi wa Google kwa miaka 9 baada ya kuwa mmoja wa Wanafunzi bora kutoka Chuo Kikuu cha Stanford. Baadaye aliajiriwa kama Mshauri wa Masuala ya Kompyuta chuoni hapo kwa mwaka mmoja
Aidha, Mtanzania huyo alikuwa kati ya Wanafunzi Bora 12 waliofaulu vizuri Mtihani wa Kidato cha 4 mwaka 2007 ambapo walipata nafasi ya kukutana na kupongezwa na Rais Jakaya Kikwete.