WAFAHAMU WAAMUZI WA YANGA NA AL AHLY

0:00

MICHEZO

Mechi kati ya Al Ahly na Young Africans itachezeshwa na Refa Djindo Houngnandande kutoka Benin, wakati mchezo wa Simba SC na Jwaneng Galaxy utakuwa chini ya usimamizi wa Refa Daniel Nii Laryea kutoka Ghana.

Refa Houngnandande kutoka Benin anakumbukwa na Young Africans kwa kuchezesha mechi yao ya ugenini kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya US Monastir, Desenmba 12 mwaka jana, ambayo wenyeji waliibuka na ushindi wa mabao 2-0, lakini pia alichezesha mchezo wa Kombe la Mataifa Afrika kati ya Zambia na Tanzania, uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 nchini Ivory Coast.

Kwa upande wa Laryea, amewahi kuchezesha mechi moja ya Simba SC ambayo ilikuwa ni ya ugenini dhidi ya RS Berkane kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, Februari 27, 2022 ambayo Simba SC ilipoteza kwa mabao 2-0 lakini pia kwenye michuano ya AFCON 2023, alichezesha mchezo kati ya Tunisia na Mali.

Marefa hao wawili wamekuwa pia na tabia ya kutovumilia Rafu na Matendo ya Utovu wa Nidhamu na pale yanapofanyika wamekuwa hawasiti kuonyesha kadi kwa wachezaji waliofanya, hii ikiwa ni alamu kwa Sadio Kanoute wa Simba SC na Khalid Aucho kwa upande wa Young Africans.

Refa Laryea mwenye umri wa miaka 36, katika mechi 21 za mashindano ya klabu Afrika ambazo amechezesha, ametoa kadi 79 ambapo nyekundu ni tatu na za njano ni 76.

Kwa upande wa Houngnandande mwenye umri wa miaka 36, amechezesha idadi ya mechi 14 za mashindano ya klabu Afrika ambapo ameonyesha idadi ya kadi 59, mbili zikiwa nyekundu na kadi 57 zikiwa za njano.

Wakati Young Africans ambayo imeshafuzu hatua ya Robo Fainali ikitakiwa kushinda ili kukaa kileleni kwa msimamo wa kundi, Simba SC yenyewe inalazimika kupata ushindi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ili ipate tiketi ya kwenda Robo Fainali.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

TEN HAG NA SANCHO WAGOMBANA ...
London Winga #JadonSancho amedai sio kweli kuwa amekuwa hapati nafasi...
Read more
BOMOA BOMOA KUANZA APRILI 12 DAR ES...
HABARI KUU Mratibu wa Miradi ya Ushirikiano Kati ya Benki...
Read more
Lionel Messi is back to the...
Argentina captain Lionel Messi is ready to return to their...
Read more
WAZIRI MKUU WA CONGO LUKONDE AJIUZULU
HABARI KUU Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,...
Read more
DJ Cuppy shared her reaction on social...
She posted a video of the text, generating curiosity and...
Read more

Leave a Reply