WATU 7 WAKAMATWA KWA KUGOMEA CHANJO

0:00

HABARI KUU

Watu saba wote Wakazi wa Kijiji cha Kalambo Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa, wamehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja Jela kila mmoja na Mahakama ya mwanzo Wilaya ya Kalambo baada ya kugoma Watoto wao wenye umri kati ya miezi 9 hadi 59 wasipewe chanjo ya ugonjwa wa Surua na Rubela wakidai chanjo sio maagizo ya Mungu.

Hukumu hiyo imetolewa February 26,2024 na Mahakimu wa Mahakama hiyo Elis Mkama na Suzy Mkinga kwa Washtakiwa hao ambao ni Abiniel Isaya (27), Misheck Simon (28), Isack Simon (26), Yona Simon (30), Efeso Peter (28), Job Simon (36) na Joshua Meshack (40)

Akitoa taarifa kuhusu hukumu hiyo leo February 27,2024, RPC wa Rukwa, Shadrack Masija amesema chanjo hiyo ilikuwa ikitolewa na Wizara ya afya katika Kijiji hicho February 18,2024, ambapo sababu ya kugomea ni imani ya dini yao ya Kanisa la Watchtower kwamba chanjo sio maagizo ya Mungu.

RPC Masija mesema “Kugomea chanjo inayoelekezwa na Serikali ni kufifisha juhudi za Serikali za kupambana na maradhi hivyo amewahimiza Wananchi wazingatie maagizo na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Serikali na wazitii Mamlaka za Serikali kwani zimewekwa na Mungu ambaye ndiye wote tunamwabudu”

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

PORTABLE EYES GRAMMY FOR BEST AFRICAN ARTIST
CELEBRITIES Nigerian singer, rapper, and songwriter, Habeeb Okikiola, popularly known...
Read more
BERNARD KAMUNGO KUTOKA KUWA MKIMBIZI NA KUWA...
<!--INDOLEADS - BEGIN--> Makala Fupi Ni MUNGU tu mwenye Mamlaka ya kumruzuku...
Read more
ROBERT LEWANDOWSKI AKATAA OFA HII YA SAUDIA...
MICHEZO Mshambuliaji wa FC Barcelona, Robert Lewandowski, amekataa mkataba mnono...
Read more
Bologna Draw by Visitors Shakhtar Donetsk
Bologna were held to a 0-0 draw by visitors Shakhtar...
Read more
30 WAYS TO BRING ROMANCE BACK TO...
LOVE TIPS ❤
See also  MILIONI 300 ZAMBAKISHA KIBU DENIS SIMBA
We always mistake romance whenever it's mentioned...
Read more

Leave a Reply