MAKALA
Kila kitu hapa duniani kina ASILI yake inayoelezea safari ya kilipotoka mpaka pale kilipo.
Wewe na mimi pia tuna asili zetu.
Hakuna kisichokuwa na asili.
Hata haya majina ya miezi 12 ya mwaka, yaani Januari hadi Decemba yana asili yake.
Niseme tu kwamba Astrology au Elimu ya Nyota ndiyo elimu inayotawala mambo mengi katika hii dunia.
Chimbuko la vitu vingi ni Astorolojia.
Kwenye masomo yaliyopita nilieleza kuwa siku 7 za wiki pia zinatokana na ¼ ya siku 28-30 za mzunguko wa mwezi kwenye Sayari ya dunia.
Week (wiki/ juma) ni matokeo ya siku 7 ambazo ni mzunguko mmoja wa mwezi kwenye Sayari ya dunia na mwezi unazunguka dunia kwa awamu nne zenye majina mwezi mwandamo, mwezi Mpevu, mwezi mchanga na mwezi kamili, kila awamu ikiwa na wastani wa siku 7!
Majina ya hizo siku 7 yametokana na Jua, Mwezi pamoja na Sayari kongwe 5.
Hii ni elimu ya Nyota, Astrology!
Miezi 12 ya mwaka pia imetokana na Astrology.
Majina ya miezi, kwa mfano mwezi Machi (March), yametokana na Jina la Sayari ya Mars. Hii ni astrology!
Rumi ambayo ndiye mtawala wa Dunia kwa muda mrefu sana pengine kuliko tawala zote, ndiye muasisi wa mifumo mingi tofauti tofauti inayoongoza dunia na maisha ya walimwengu kwa ujumla.
Sehemu kubwa ya dunia mpaka leo kisiasa, kiroho/kidini, kiuchumi, kiutamaduni nakadhalika, huongozwa na mifumo ya Roman Empire!
Kalenda yetu ya miezi 12 ambayo inatumika sehemu kubwa ya dunia inaitwa Kalenda ya Gregory (Gregorian calendar) aliyekuwa Papa wa Roma kwenye Karne ya 16.
Kalenda hii ilitokana na Kalenda ya Julius Kaisari ambaye alikuwa mtawala wa himaya ya Roma. Iliitwa Julian calendar.
Julius Kaisari ndiye mtawala mwenye historia kubwa sana pengine kuliko mtawala yeyote wa Roma ya kale na dunia kwa ujumla.
Historia yake ina mambo mengi ambayo nitayaeleza kwenye makala zijazo.
Ni huyu Julius ambaye aliibadilisha kalenda kongwe ya Wakaldayo iliyokuwa na miezi 10 (siku 304) kuwa miezi 12 (siku 365¼ au 366) ili iendane na mzunguko wa dunia katika kulizunguka Jua.
Dunia ulizunguka Jua kwa siku 366 sawa na miezi 12 ambayo imepewa majina ya Nyota.
Ndio maana Nyota ya mtu hutambuliwa kwa kuangalia siku na mwezi aliozaliwa.
Kama ulizaliwa let’s say tarehe 26/3 maana yake Nyota yako ni ile inayotawaliwa na Sayari ya Mars, ambayo ni Aries (Nyota ya Punda)
Kabla ya Julian calendar, ambayo baadaye ilifanyiwa mabadiliko na Papa Gregory XIII, mwezi Oktoba 1582, kalenda iliyokuwepo ilitumia majina ya namba za kawaida za Kirumi kuanzia namba moja hadi kumi.
Mwezi wa kwanza hadi wa 10 ulitajwa kwa majina yafuatayo:
Martius,
Aprilis,
Maius,
Junius,
Quintilis,
Sextilis,
September,
October,
November na
December.
Niliishia pale niliposema kwamba kabla mwaka haujawa na miezi 12 (siku 366) ulikuwa na miezi 10 tu sawa na siku 304!
Kwamba kabla ya Julian calendar, ambayo baadaye ilifanyiwa mabadiliko kidogo na Papa Gregory XIII, mwezi Oktoba 1582, kalenda iliyokuwepo ilitumia majina ya namba za kawaida za Kirumi kuanzia namba moja hadi kumi.
Mwezi wa kwanza hadi wa 10 ulitajwa kwa majina yafuatayo:
✍️Martius (mwezi wa 1),
✍️Aprilis (mwezi wa 2)
✍️Maius (mwezi wa 3)
✍️Junius (mwezi wa 4)
✍️Quintilis (mwezi wa 5)
✍️Sextilis (mwezi wa 6)
✍️Septembrus (mwezi wa 7)
✍️Octoburus (mwezi wa 8)
✍️Novemburus (mwezi wa 9) na ✍️✍️Decemburus (mwezi wa 10)
Mnamo karne ya 7 Kabla ya kuzaliwa Kristo, iliamuliwa kurekebisha Calendar hiyo ili kuifanya iendane na mzunguko wa dunia kulizunguka Jua ambapo Dunia hulizunguka Jua mara 12 kwa mzunguko wa wastani wa siku therathini – therathini.
Kwa hiyo ilibidi ziongezwe siku 60 ambazo ni sawa na miezi miwili ambayo waliipa majina ya Janus na Februus kwa heshima ya miungu yao.
Julius Kaisari akiwa madarakani mnamo mwaka 45 Kabla ya Kristo, alitangaza kusheherehekea mwanzo wa mwaka mpya siku ya kwanza ya mwezi Janus (January) yaani Januari mosi 45.
Kwa hiyo itoshe kusema maadhimisho ya kwanza ya mwaka mpya, yanayozingatia utaratibu wa Januari mosi yalianzishwa na Kaisari Julius tarehe 1 Januari, mwaka wa 45KK.
Kwa hiyo sio kweli kwamba mwaka mpya huanza tarehe 1 Januari bali mwaka huanza mwezi Machi.
Kuanza mwezi Januari mosi ni utashi wa Mfalme au Kaisari Julius katika kumuenzi mungu wao Janus!
Kabla ya mabadiliko hayo yaliyofanywa mwaka 45 KK na Kaisari Julius, majina ya miezi yalikuwa kama ifuatavyo:
✍🏻Mwezi wa kwanza uliitwa Mars (March) kwa heshima ya Sayari ya Mars ambayo kwa Warumi iliheshimiwa kama mungu, naam mungu wa vita!
✍🏻Mwezi wa 2 uliitwa Aprilis, yaani ‘mbili’ ambao sisi tunaita April.
✍🏻Mwezi wa 3 uliitwa Maya kwa heshima ya mungu mke Maiesta (mungu wa ardhi na rutuba)
Kabla ya hapo mwezi huu uliitwa Maius kumaanisha 3 ambao sisi leo tunaita May (Mei)
✍🏻Mwezi wa 4, ulipewa jina la mungu mke aitwaye Juno aliyekuwa mke wa mungu Jupiter.
Sisi tunaita June.
✍🏻 Mwezi wa 5 ulioitwa Quintilis kumaanisha ‘tano’ ulipewa jina ‘Julius’ kwa heshima ya Kaisari Julius, ambao leo sisi tunauita mwezi July/ Julai.
✍🏻Mwezi wa 6 uliitwa Sextilis kumaanisha namba sita, lakini ukabadilishwa na kuitwa Augustus kwa heshima ya Mfalme Augustus mpwawe Kaisari Julius.
Mwezi huu sisi ndio leo tunauita August au Agosti.
✍🏻Mwezi wa 7 (Septemburus), wa 8 (Octoburus) wa 9 (Novemburus) na wa 10 (Decemburus) humaanisha namba husika; yaani 7, 8, 9 na 10 kwa Kirumi.
Miezi hiyo sisi ndo tunaita September, October, November na December.
Mwezi wa 11 na wa 12, ndiyo iliyoongezwa na kupewa majina ya miungu Janus na Februus kama nilivyosema awali, ambayo leo sisi tunaita January na February.