ATEKWA NA WENZAKE KWA KUWATAPELI MADAWA YA KULEVYA

0:00

HABARI KUU

WATU wanaodhaniwa kuwa vigogo wa mtandao wa dawa za kulevya wamemteka mshirika wao na kumzungusha maeneo mbalimbali ya Jiji la Tanga wakishinikiza kulipwa shilingi milioni 50 au arudishe mzigo wa dawa zinazodhaniwa kuwa za kulevya ambazo walimkabidhi mshirika waliyemteka.

Tukio la kutekwa kwa mtu huyo aliyetajwa kwa jina la Muki Kizinga lilitokea Februari 14 mwaka huu katika Halmashauri ya Jiji la Tanga na Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga Almachius Mchunguzi amethibitisha tukio hilo

Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Almachius Mchunguzi amesema baada ya polisi kupokea taarifa za kutekwa kwa Kizinga walianza uchunguzi na kufanikiwa kumkamata Khalid Mwarangi aliyedaiwa kumteka Kizinga.

Alisema, chanzo cha mtu huyo kutekwa ni watekaji kudai walipwe shilingi milioni 50 au kurudishiwa dawa zinazodhaniwa kuwa za kulevya ambazo walimkabidhi mtekwaji kuzisafirisha kwa lengo la kuuza.

Kamanda Mchunguzi alisema watekaji walikuwa wakimshinikiza Kizinga kuwarejeshea dawa zao au kuwalipa shilingi milioni 50 huku mtekwaji huyo akiwaeleza kuwa alikamatwa Ethiopia.

Kwa mujibu wa Kamanda Mchunguzi, Mwarangi ambaye ni mkazi wa Kimara Jijini Dar es Salaam anashikiliwa na polisi ambapo alikutwa akiwa na Kilogram 25 za dawa zinazodhaniwa kuwa ni za kulevya huku akiwa na hati mbili za kusafiria.

Aidha mtu aliyekuwa ametekwa naye amepatikana akiwa salama.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Muhammad Mukhbar Rais mpya wa Iran
HABARI KUU Kiongozi wa ngazi ya juu nchini Iran, Ayatollah...
Read more
THE FIVE LOVE LANGUAGES
LOVE TIPS ❤ THE FIVE LOVE LANGUAGESMany people have wrongly...
Read more
JE KUONEANA WIVU NI SEHEMU YA MAPENZI?...
Makala Fupi
See also  AFARIKI AKIFANYA UPASUAJI WA KUONGEZA MAKALIO
Mapenzi yananoga wivu unapokuwa ndani yake. Ukitathimini...
Read more
HENDERSON MBIONI KUREJEA ULAYA
MICHEZO Klabu ya Juventus ya Italia imeripotiwa kufanya mazungumzo na...
Read more
ARSENAL YATWAA NGAO YA JAMII KWA KUICHAPA...
London Arsenal imetwaa Ubingwa wa Ngao ya Jamii baada ya kuifunga...
Read more

Leave a Reply