HABARI KUU
Bunge la Ghana limepitisha Muswada mkali dhidi ya watu wanaojitambulisha kwa jinsia na mahusiano yasiyokubalika kisheria.
Chini ya muswada huo, mtu yeyote atakayekutwa na hatia hiyo atahukumiwa kifungo cha hadi miaka mitatu jela.
Aidha, watakaoanzisha au kuyafadhili makundi ya watu wa aina hiyo watahukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.
Pamoja na hayo, wale wote watakaohusika na kuhamasisha tabia na vitendo hivyo wakilenga watoto watahukumiwa kifungo cha miaka kumi jela.
Muswada huo pia umehimiza wananchi kuwaripoti kwa Mamlaka wale wote wanaojihusisha na tabia na vitendo hivyo ili waweze kuchukuliwa hatua stahiki.
Muswada huo ulioungwa mkono na vyama vikubwa viwili vya nchini humo, utaanza kutumika ikiwa Rais Nana Akufo-Adoo atatia saini na kuufanya kuwa sheria.
Rais Akufo-Addo alikwisha ahidi ya kuwa yupo tayari kutia saini muswada huo ikiwa Waghana walio wengi watamtaka kufanya hivyo.