MICHEZO
Mchezaji Heritier Luvumbu Nzinga amesaini makataba wa msimu mmoja kwa ajili ya kuitumikia klabu ya AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Nyota huyo amesaini mkataba huo mbele ya Rais wa klabu ya AS Vita Club Amadou Diaby.
Hata hivyo, vipengele vya mkataba kati ya mchezaji huyo na mwajiri wake mpya havijawekwa wazi lakini winga huyo amesaini mkataba wa awali wa msimu wa 2024-2025.
Klabu ya AS Vita Club itaanza awamu yake ya mchujo Jumapili ijayo Machi 3 dhidi ya FC les Aigles du Congo ambayo pia imeijiimarisha kwa kuwaleta wachezaji wachache, akiwemo Mukoko Amale.
Kumbuka Luvumbu alirejeshwa nchini baada ya kuwekewa vikwazo na Shirikisho la Soka la Rwanda ambalo lilimkosoa kwa tabia mbaya uwanjani.
Katika ardhi ya Rwanda mnamo Februari 11, Luvumbu alisherehekea bao lake kwa ishara ya kukemea mauaji mashariki mwa DRC sambamba na ukimya wa jumuiya ya Kimataifa.