HABARI KUU
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameitangaza ratiba ya maziko ya Rais wa mstaafu Ally Hassan Mwinyi itakayoanza leo saa tano na nusu asubuhi kwa mwili kuondoka nyumbani kwake Mikocheni kuelekea Msikiti Mkuu wa BAKWATA Kinondoni ambako Sheikh Dkt. Abubakar Bin Zuber Bin Ali ataongoza swala ya Ijumaa na taratibu zote za kidini.
“Saa 8:00 Mchana, mwili wa utaelekea Uwanja wa Uhuru na kuanzia saa 8:30 mchana ni dua na maombi kutoka kwa Viongozi wa Dini na salamu za rambirambi kutoka kwa Viongozi mbalimbali, pia Viongozi na Wananchi mbalimbali kutoa heshima za mwisho”
“Saa 11:00 jioni mwili utaondolewa uwanja wa Uhuru kuelekea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, saa 11:30 Jioni Wananchi wa Zanzibar na maeneo mengine ya Unguja wataupokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume” ——— Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.