0:00
HABARI KUU
Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limesema Marehemu Martin Chacha aliyekuwa akifanya kazi ya udereva katika Kampuni ya ASAS alikutwa na umauti akiwa Gerezani akitumikia kifungo tofauti na taarifa za awali zilizosambazwa mitandaoni zikisema mtu huyo aliuawa kwa kipigo baada ya kuiba Mafuta.
Martin Chacha alihukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela baada ya kukutwa na hatia ya kuiba mafuta aina ya Dizeli Lita 383 mali ya kampuni ya ASAS aliyokuwa akiifanyia kazi.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi amesema Martini Chacha alituhumiwa kwa tuhuma za wizi na alihukumiwa tarehe 20 Februari 2024.
Related Posts 📫
HABARI KUU
MJANE wa marehemu Harry Roy Veevers, raia wa...
Ugumba unaweza kuwa wasiwasi kwa wanaume pia kama kwa wanawake....
The Nike Flight Premier League ball will enjoy its first...