WAMILIKI WA HOSPITALI ZA BINAFSI NA SERIKALI WAKUBALIANA

0:00

HABARI KUU

Uongozi wa Bodi ya Wamiliki wa Vituo vya Afya vya Binafsi APHFTA na Jumuiya ya Wamiliki Hospitali Binafsi Zanzibar ZAPHOA, umefikia uamuzi wa kurejea kwenye meza ya mazungumzo na Serikali sambamba na kurejesha huduma za Afya zilizositishwa kwa Wanachama wa NHIF wakati mazungumzo na Serikali yakiendelea.

Taarifa ya APHFTA kupitia kwa Mwenyekiti wake Dkt. Egina Makwabe imebainisha kuwa imefikia uamuzi huo kufuatia Serikali kuonyesha utayari wa kurudi katika meza ya mazungumzo kupitia mawasiliano yanayoendelea kati ya Serikali na APHFTA.

“Tunawataarifu na kuwasihi Watoa Wuduma kurejesha huduma hizo kuanzia 3/3/2024 hadi hapo tutakapowatangazia vinginevyo.” imesema taarifa hiyo.

APHFTA imesisitiza kwamba lengo lake ni kutoa huduma bora za afya katika mazingira ambayo yanazingatia hali ya soko na uhalisi wa gharama za uendeshaji za wamiliki wa vituo vya afya na hospitali. “Kamwe, dhamira yetu si kuwaumiza wananchi wahitaji ambao ni wanachama wa NHIF” imesema.

“Uamuzi huu mgumu tunaouchukua ni kielelezo cha nia yetu njema na dhamira yetu safi ya kutafuta suluhu ya kudumu itakayowaoendelea wananchi adha ya kupata huduma za afya katika vituo vyetu, na kutupunguzia wamiliki gharama za utoaji huduma na uendeshaji.”

Kamati maalum ya APHFTA itaundwa ili kushiriki majadiliano hayo ya kurekebisha bei zilizoleta mgogoro mkubwa.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Christ Embassy church in Lagos erupted by...
On Sunday morning, a fire erupted at the Christ Embassy...
Read more
UFARANSA YAICHAPA GIBRALTAR 14 ...
MICHEZO Timu ya Taifa ya Ufaransa imeweka rekodi ya ushindi...
Read more
Burna Boy goes into MOVIE PRODUCTION
CELEBRITIES Grammy-winning singer, Damini Ogulu, aka Burna Boy is about...
Read more
Pep Guardiola says ‘I’m not good enough’...
MANCHESTER, England 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 — Pep Guardiola declared himself “not good...
Read more
CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa...
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Leo...
Read more
See also  DC apiga marufuku wanafunzi kuchezwa ngoma

Leave a Reply