MICHEZO
Klabu ya Barcelona imemuondoa Dani Alves kwenye orodha ya wachezaji ambao walikuwa wanaheshimika kama magwiji wa klabu katika historia kwenye tovuti rasmi ya klabu ya Barcelona.
Ingawa FC Barcelona haijatoa maoni rasmi, inaaminika kuwa kitendo hicho cha kumuondoa Alves kwenye tovuti kinaashiria kuwepo kwa tahadhari ndani ya klabu kuhusiana na hali anayokumbana nayo Mbrazil huyo kwa sasa baada ya kupatikana na hatia ya unyanyasaji wa kijinsia na kusweka jela kwa kifungo cha miaka 8 na nusu.
Akiwa Barcelona Dan Alves alishinda mataji mbalimbali ambayo yalichochea kazi yake katika umaarufu wa soka. Kando na kuwa mwanasoka hodari, alikonga nyoyo za mashabiki kwa kunyakua mataji Matatu ya Ligi ya Mabingwa, Matatu ya UEFA Super Cups, Matatu ya Kombe la Dunia la Klabu.
Kwa sasa, Dani Alves hatakuwepo tena kwenye tovuti na katika sehemu ya wachezaji wa kihistoria wa Blaugrana, hata hivyo bado haijafahamika iwapo klabu hiyo inaweza kubadilisha uamuzi huo kati yake na mchezaji huyo wa zamani.