EMMERSON MNANGAGWA APIGWA VIKWAZO NA MAREKANIimg

0:00

HABARI KUU

Marekani imewawekea vikwazo watu tisa 9 nchini Zimbabwe akiwemo Rais wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa, mke wake, Auxillia Mnangagwa, Makamu wa Rais, Constantino Chiwenga, Waziri wa Ulinzi, Mkuu wa Upelelezi wa Zimbabwe na Patrick Chinamasa Mweka Hazina wa chama cha kisiasa cha Zanu PF.

Pia Marekani imeyawekea vikwazo Makampuni matatu ya kibiashara ya Zimbabwe.

Marekani inawashutumu viongozi hao kuhusika katika ukiukwaji wa haki za binadamu,rushwa,utekaji wa watu na unyanyasaji uliopitiliza.

Vikwazo hivyo ni pamoja na kukamatwa kwa nyumba zao zilizopo kwenye ardhi ya Marekani na kutoruhusiwa kuingia nchini humo.

Hadi kufikia sasa uongozi nchini Zimbabwe haujatangaza kitu chochote kuhusiana na hatua hiyo.


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  ARIEL HENRY AJIUZULU KUWA WAZIRI MKUU WA HAITI
Don't miss out!
Invalid email address

By Mujuni Henry

JUNIITV

Please disable your adblocker or whitelist this site!

         banner                            

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading