SABABU YA DUBE KUOMBA KUONDOKA AZAMimg

0:00

MAKALA

Klabu ya Azam imethibitisha kupokea barua ya PRİNCE DUBE akiomba kuondoka kwenye klabu hiyo. Taarifa ya klabu inasema Azam FC wamemjibu na kumwambia anaweza kuondoka ila kwa kufikiwa kwa vipengele vya mkataba, yani kama klabu nyingine au yeye mwenyewe anaweza kuilipa Azam FC pesa waliyoweka kwenye mkataba kama mchezaji anataka kuvunja mkataba au timu kumnunua “buy out clause”. Dube ana mkataba wa miaka 2 na miezi 6 kwenye mkataba wake unaomalizima 2026.

NYUMA YA PAZIA NINI KINAMUONDOA DUBE AZAM FC

Dube amekuwa akiweka shinikizo la kutaka kuondoka kwa muda mrefu tangu wakati wa Pre-season na kuna klabu ya Kariakoo imekuwa ikimhitaji kwa udi na uvumba baada ya kuondokewa na mfungaji wake mahiri aliyeenda kutafuta malisho kwingineko barani Afrika

Dube ambaye hayuko pia kwenye mahusiano mazuri na kocha mkuu Yusuf Dabo amekuwa akisumbuliwa sana na simu za Kigogo wa timu hiyo ya Dar es Salaam tangu wakiwa Pre-season na kwakuwa hayuko kwenye mahusiano mazuri na Dabo anaona njia ya kumtia adabu ni kuondoka na kujiunga Kariakoo.

Wachezaji wenzie wamewahi kumsihi asiondoke ili wapambanie ubingwa lakini majibu yake ni viongozi hawamheshimu kwakuwa wameshamzoea kakaa sana na kocha Dabo hawaelewani njia pekee ni kuondoka tu.

Hali ilivyo Azam FC watamgomea Dube msimu huu nadhani baada ya hapo uzoefu unaonyesha watamruhusu aende anakotaka pengine kwa pesa kidogo sana nje ya kile cha kwenye mkataba. Waliwahi kuondoka Mrisho Ngassa, Ramadhan Chombo “Ridondo” kwa mtindo kama huu au unaokaribiana, hata usajili wa Salum Abubakar Salum “Sureboy”.

Nadhani Dube na klabu inayomhitaji wanapaswa kuwa na subra kiasi tu, mabosi wa Azam FC huwa hawapendi zogo na timu za Kariakoo analotaka litakuwa ni suala la muda tu.

Ningeshangaa sana watu wakae na Jose au Fredwaaa na Prince yuko Chamazi? Lazima tu ingekuwa hivi katika hali ya kawaida LAZIMA. Mwenye Kisu kikali atakula nyama. Lakini pia wachezaji wanapenda kucheza mashindano makubwa ya Afrika na kufika mbali, wanapenda kushinda vikombe vya ligi pia. Kwahiyo wanashawishika kirahisi kwakuwa Kariakoo wanafanikiwa.

See also  Mashtaka Yanayomkabili Kijana KOMBO MBWANA

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Man United boss Amorim coy over reason...
MANCHESTER, England 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 — Marcus Rashford and Alejandro Garnacho were...
Read more
CHIELLINI AMESTAAFU KUCHEZA MPIRA
NYOTA WETU. Beki wa zamani wa Juventus na Timu ya...
Read more
Hot model on bikini lingerie around places
Mattis nunc sed blandit libero volutpat sed. Egestas pretium...
Read more
BENKI KUU YA TANZANIA IMEPIGA MARUFUKU KUWEKA...
HABARI KUU BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeonya watu ambao...
Read more
Yul Edochie’s ex-wife, May, joins Nollywood
May, the estranged wife of Nollywood actor Yul Edochie, has...
Read more

Leave a Reply