ZUCHU AFUNGIWA KUFANYA MZIKIimg

0:00

NYOTA WETU

Baraza la Sanaa, Sensa, Filamu na Utamaduni la Zanzibar, limemfungia msaanii wa kizazi kipya Zuhura Othman Masoud maarufu Zuchu kuendesha shughuli zote za sanaa visiwani Zanzibar sambamba na kupiga marufuku redio na televisheni za visiwani humo kupiga nyimbo zake kwa kipindi cha miezi sita.

Hatua hiyo imekuja baada ya tukio la Februari 24 mwaka huu Zuchu wakati akitumbuiza katika usiku wa Fullmoon Kendwa Mkoa wa Kaskazini Unguja kudaiwa kuimba nyimbo, kutoa matamshi na kuonyesha ishara mbaya ambazo ni kinyume na maadili ya kizanzibari.

Akizungumza leo Machi 5, 2024 ofisini kwake na waandishi wa habari, katibu mtendaji wa baraza hilo, Omar Abdalla Adam amesema baraza limemfungia kwa kipindi cha miezi sita kuanzia sasa.

“Baraza lina wajibu wa kusimamia mila, silka desturi na utamaduni wa Mzanzibari, kwa hiyo linatamka rasmi kumfungia msanii Zuhura Othman Soud (Zuchu) kufanya shughuli yoyote ya sanaa kwa Zanzibar kwa kipindi cha muda wa miezi sita kuanzia leo Machi 5, 2024,” amesema.

Amesema wanafanya hivyo kutokana na tabia yake kuimba nyimbo ambazo hazina maadili, hazifuati misingi na hazina afya njema kwa jamii ya Wazanzibari.

Pia, amesema licha ya msanii huyo kutokuwa na usajili Zanzibar lakini amekuwa akiendesha shughuli zake za sanaa bila kupata kibali.

Mbali na adhabu hiyo, pia msanii huyo ametakiwa kulipa faini ya Tsh milioni moja kwa Baraza la Sanaa na aandike barua ya kuomba radhi na kuthibitisha kwamba hatafanya kosa hilo ndani ya kipindi alichofungiwa.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

How the stars aligned to make micropayments...
Why Dropp, why now, and what does it mean for...
Read more
MAOMBI YA UPIMAJI DNA YAONGEZEKA ...
MAGAZETI
See also  Protest: Education Minister urges students to remain on campus
Karibu Mtanzania kwenye magazeti ya leo kwenye mbao za...
Read more
DIDDY MAKES ADVANCES TO MAKE ARTIST...
OUR STAR 🌟 U.S. rapper Sean “Diddy” Combs is enmeshed...
Read more
Douglas Kanja Takes Oath as New Inspector...
Inspector General of the National Police Service Douglas Kanja officially...
Read more
MKUU WA MKOA MSTAAFU AKAMATWA KWA...
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia aliyekuwa Mkuu wa Mkoa...
Read more

Leave a Reply