MICHEZO
Bondia Anthony Joshua ametamba kumpiga mpinzani wake Francis Ngannou kwa ‘KO’ kwenye pambano la uzito wa juu litakalofanyika Saudi Arabia, mwishoni mwa juma lijalo.
Joshua kwa sasa ameshinda mapambano matatu mfululizo na hivi karibuni alimshinda Otto Wallin raundi ya tano Desemba mwaka jana.
Joshua anatarajia kupata ushindani tofauti kutoka kwa Ngannou kwenye pambano hilo lisilo la ubingwa, kwani nyota huyo wa kareti alimpiga Tyson Fury kwenye pambano lake la kwanza la ndondi Oktoba mwaka jana.
“Ninaamini naweza kumpiga kwa KO. Hakika, ningependa kumpiga kwa KO na kutuma salamu.” amesema Joshua
“Kimwili, najisikia ni mwenye nguvu, najisikia vizuri. Najiona nina nguvu za kutosha kukamilisha kazi na kiakili niko tayari kwa vita.
“Kiakili sihofii sana kuhusu mpinzani wangu na nikiangalia nini mpinzani wangu anaweza kufanya naona naweza kuvuka ushindani huu. Nafanya bidii kuongeza kiwango changu na nitaonesha kila kitu nilichonacho.”